NI KAULI YAKE MAMA JANET MAGUFULI KATIKA MAADHIMSHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YENYE KAULI MBIU ISEMAYO "KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA TUIMARISHE USAWA WA KIJINSIA NA UWEZESHAJI WA WANAWAKE VIJIJINI "
Mashirika ya Umma na Sekta binafsi kote nchini yametakiwa kuhakikisha yanashirikiana bega kwa bega na Serikali katika kumuwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi na kimaendeleo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Janet Magufuli, Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa Mageni rasmi siku ya maadhimisho ya mwanamke duniani yenye kauli mbiu isemayo "Kuelekea Uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa Jinsia na uwezeshaji wa wanawake vijijini."
Amesema kufuatia kauli mbiu hiyo wanawake wanatakiwa kujengewa uwezo ikiwemo elimu ya ujasiriamali, mafunzo, ili kupata mbinu za kuwekeza, mitaji pamoja na maeneo kwa lengo la kumsaidia mwanamke kujikwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa lengo la siku ya wanawake duniani ni kutukumbusha harakati na mafanikio yaliyokwisha fanyika katika kumkwamua mwanamke dhidi ya unyanyasaji, hali duni, kutelekezwa na kuhakikisha haki yake inapatikana, inaheshimiwa na kuenziwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Mh Paul Makonda alipotoa nasaha zake wakati wa maadhimisho hayo amesema wanawake wa Mkoa wa Dar Es Salaam wanajitahidi Sana katika kuhakikisha wanaendana na kasi iliyopo ya uchumi wa viwanda.
Amebainisha kuwa katika Mkoa wake kunajumla ya vicoba 2748 vyenye mtaji wa takribani bilioni 10.78 ambavyo vinaendeshwa na wanawake.
Aidha amebainisha kuwa katika mkoa wake unajumla ya idadi ya watu milioni 6, na kati ya hao wanawake ni wengi kuliko wanaume, hivyo ni jeshi kubwa ambalo likiwezeshwa linaweza.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City yamehudhuriwa na Makatibu tawala wa Wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam, Wakuu wa Wilaya, Watendaji wa Taasisi za Serikali, Viongozi wa CWT, pamoja na wanawake wa Mkoa wa Dar Es Salaam .
Imetolewa na
Kitengo chá Uhusiano na Habari
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.