Kiwango cha ufubazaji maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ndani Manispaa ya Kinondoni imeendelea kuimarika ukilinganisha na idadi ya waathirika wanaotumia dawa.
Mratibu wa Ukimwi wa Manispaa ya Kinondoni, Dkt. Emmanuel Paul Biya, akiwasilisha mada ya hali ya Maambukizi ya Ukimwi kwa Wajumbe wa CMAC Julai 24, 2024 alisema hadi sasa asilimia 97.4 ya Wanaume na Wanawake wamefubaza maambukizi kati ya asilimia 98.4 ya Wanaume na asilimia 99 ya Wanawake wanaotumia Dawa. Hadi Juni, 2024 jumla ya watu 42,458 wanatumia dawa za kufubaza maambukizi ya Ukimwi.
Mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati hiyo ya Kudhibiti Ukimwi ngazi ya Manispaa (CMAC) yamefunguliwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Josephat Rwegasira. Mafunzo hayo yamefadhiliwa na USAID kupitia Mradi wa EPIC.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.