Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Joseph Rwegasira, amempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanikisha maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Rwegasira ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la Manispaa ya Kinondoni leo Julai 07, 2023 ambapo pia alipata fursa ya kutembelea biashara za wajasiriamali wa Manispaa ya Kinondoni.
"Nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kufanikisha maonesho haya. Yamefana kwa kiwango kikubwa", alisema. Sambamba na pongezi hizo, pia Mheshimiwa Rwegasira ametoa rai kwa wakazi wa Dar es Salam na mikoa jirani kufika katika viwanja hivyo vya maonesho kwa ajili ya kupata huduma, elimu na bidhaa mbalimbali.
"Nawashauri wananchi ambao hawajatembelea banda la Manispaa ya Kinondoni wafike kwa ajili ya kupata elimu, huduma na bidhaa mbalimbali," alisema na kuongeza kuwa, "pia nawaomba Waheshimiwa Madiwani ambao hawajafika kwenye maonesho haya waje watembelee".
Mheshimiwa Rwegasira ambaye ni Diwani wa Kata ya Makongo, kadhalika amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa, Bi. Hanifa Suleiman Hamza, na Watumishi kwa kazi nzuri ya maandalizi na ushiriki wa maonesho hayo. "Nampongeza sana Mkurugenzi kwa kazi nzuri na ushiriki wa maonesho haya", alisema.
Alisema, "nimeshuhudia wananchi wakipata Huduma mbalimbali kupitia mfumo wa TAUSI. Hongereni sana".
Katika Hatua nyingine Kituo Cha Televisheni cha Channel Ten mapema leo kilitembelea banda la Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Manispaa katika Maonesho hayo. Taarifa kamili ya ujio wa Channel Ten itakujia leo usiku kuanzia saa mbili.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.