Manispaa ya Kinondoni leo imepongezwa kwa kuvuka msimu wa mvua bila ya kuwa na mlipuko wa kipindupindu kwenye maeneo yake licha ya kuwa na maeneo yenye madimbwi yasiyoepukika.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Ali Hapi katika mkutano ulioshirikisha wenyeviti wa serikali za Mitaa, watendaji wa Kata na Mitaa, Maafisa Afya pamoja na Maafisa kutoka idara ya Usafishaji na Mazingira uliofanyika leo.
Amesema lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini ya hali ya Afya na usafi wa Mazingira kwenye Manispaa yetu na ndio maana tumewaita wadau wanaohusika na sekta hii.
Ameongeza kuwa ni vema watu wote tuungane tushirikiane na kutoa msukumo mpya katika swala hili la usafi ili mazingira yetu yawe safi zaidi.
Amebainisha kuwa katika kipindi cha msimu wa mvua kazi iliyofanyika ni kubwa ya kuhakikisha dawa inapulizwa kwenye maeneo hatarishi na kupelekea kutokuwa na milipuko ya magonjwa ya kipindupindu.
"Msimu huu wa mvua tumepambana sana, na Mkurugenzi pamoja na mganga Mkuu, tumefanya kazi kubwa ya kuwahimiza watu kwenye Kata hizi kupuliza dawa. Na mimi naomba niwapongeze sana Mkurugenzi na Mganga Mkuu, pamoja na timu yake, na wote waliofanya ile kazi, hatujapata a serious case ya kipindupindu mwaka huu. "Alisisitiza Hapi.
Amewataka watendaji wa Kata, watendaji wa Mitaa pamoja na wenyeviti kuwajibika katika Kata zao ili kuhakikisha ufanisi unakuwepo katika maswala ya usafi na Mazingira.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.