Manispaa ya Kinondoni leo imepokea ujumbe wa Baraza la Madiwani kutoka Halmashuri ya Manispaa ya Ilemela waliokuja kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika maswala ya utendaji.
Ujumbe huo wa Baraza la Madiwani chini ya Mstahiki Meya wao Mh. Renatus Mulunga uliambatana pia na watendaji wa idara mbalimbali kutoka Halmashauri hiyo wakiwemo idara ya sheria, Afya, Utumishi, Mipangomiji, pamoja na mwandishi wa Mikutano.
Akiwakaribisha Kinondoni hapo Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh Benjamin Sitta amesema amefurahishwa sana na ujio wao kwani kwa kufanya hivyo ni hatua katika kujifunza na pia ni njia pekee katika kubadilishana uzoefu katika utendaji.
Mada zilizowasilishwa na Manispaa ya Kinondoni kwa wageni hao ni pamoja na Jinsi ya kupanga, kupima na kuendeleza miji ili kudhibiti makazi holela.
Mada nyingine ni mikakati inayotumiwa na Manispaa ya Kinondoni katika kukusanya, na kuondosha taka ngumu, vyanzo vya mapato vya Halmashauri pamoja na mbinu zitumiwazo kukusanya mapato.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Aron Kagurumjuli amesema ujio wao umeonyesha imani kubwa kwa wanakinondoni, na kwamba wamefanya vema kuja kujifunza kwani ndio Halmashauri Mama Tanzânia kwa maswala ya ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo.
Amesema kwa ujio wao ni mwanzo mzuri wa kujenga mahusiano ya kiutendaji yenye tija na yatakayoleta manufaa kwa wengine hasa ikizingatiwa Halmashauri lazima ikusanye mapato.
Katika hatua nyingine Manispaa ya Ilemela imefurahishwa na mbinu zinazotumiwa na Manispaa ya Kinondoni katika kukusanya Mapato ambapo hutumia mfumo wa Kielektroniki
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.