Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta leo amekuwa mgeni rasmi kwenye makabidhiano ya shule ya Sekondari yenye thamani ya zaidi ya milioni 800 kutoka kwa Shirika la Good eighbours na Kampuni ya kutengeneza magari ya KIA motors kutoka nchini Korea.
Akipokea shule hiyo kutoka kwa wafadhili Meya Sitta amesema Manispaa imefurahishwa na swala zima la kukabidhiwa shule hiyo ikiwa na vitendea kazi vyote vya muhimu vinavyompasa mwanafunzi kusoma ikiwemo vyumba vya madarasa vinane, maabara mbili, maktaba moja, ofisi za waalimu,uwanja wa michezo pamoja na vifaa vya fizikia na kemia.
Amesema ni vema Mwanafunzi akahakikisha anatumia vema fursa hiyo na kusoma kwa bidii, juhudi na maarifa ili aweze kufikia malengo aliyoyakusudia katika elimu.
Ameongeza kuwa Serikali ya sasa ni Serikali ya viwanda hivyo inahitaji vijana wasomi ili waweze kuviendesha viwanda hivyo bila kutegemea watu kutoka nje.
Akikabidhi shule hiyo kwa Manispaa ya Kinondoni mwakilishi wa Kampuni ya KIA motors kutoka Korea ndugu Jin Dae Hyung amesema shule hiyo imejengwa kwa viwango vya juu, na ni matumaini yake kuwa itasaidia vijana wengi kupata elimu inayokidhi viwango bila shida yeyote.
Katika hatua nyingine Afisa Elimu wa Manispaa hiyo Bw Rodgers Shemwelekwa amesema Manispaa ya Kinondoni inayo wajibu wa kulipia huduma muhimu za shuleni hapo kama vile ulinzi, huduma ya umeme na maji kwa Mwaka mzima .
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.