Magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, saratani na kisukari yamekuwa chanzo cha vifo na usumbufu kwa wananchi wa maeneo ya mijini ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam.
Mienendo isiyofaa katika maisha ikiwemo kutokufanya mazoezi, ulaji usiofaa, ulevi na uvutaji sigara imekua ni sababu kuu za kuchangia kuenea kwa magonjwa yasiyoambukiza.
Serikali inaendelea kutoa elimu ya kutosha ya namna bora ya kukabiliana na magonjwa hayo na kuendelea kuboresha na kuongeza miundombinu mbalimbali ya afya.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Godwin Gondwe akipatiwa maelekezo ya ujazaji kadi maalum ya ufuatiliaji wa afya hususani magonjwa yasioyoambukiza wakati wa maadhimisho hayo mapema leo.
Kupitia wiki hii ya maadhimisho ya magonjwa yasiyoambukiza kwa Mkoa wa Dar es Salaam wananchi wanapata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali bure na kupatiwa ushauri wa kitaalamu.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.