Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeungana na Watanzania kote nchini kusikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkesha wa miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uwanja wa Tanganyika Packers Kawe ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko.
Katika hotuba hiyo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ilitaja mambo matatu muhimu yaliyopelekea uwepo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais Dkt. Samia amesema hayo Aprili 25, 2024 wakati akilihutubia Taifa saa 3:00 ikiwa ni hotuba maalum kuelekea siku ya maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao huadhimishwa kila ifikapo tarehe 26 Mwezi wa 4 kila mwaka.
Moja ya mambo muhimu aliyoyasema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ni, Muungano ulitokana na Imani na Dhamira kubwa waliyokuwa nayo Waasisi wetu Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume waliojenga umoja na mshikamano baina ya Nchi hizi mbili.
Pili waasisi wetu walitanguliza mbele maslahi ya Wananchi wao ambao umekuwa ukileta matokeo chanya na kurahisisha kuwepo kwa Muungano huo.
Na mwisho Mhe. Rais Dkt. Samia alisema kuwa, uwepo wa ukaribu, maelewano mazuri na undugu wa kihistoria uliokuwepo baina ya Tanganyika na Zanzibar ulirahisisha zoezi hilo la kuungana baina ya pande hizi mbili hivyo ni muhimu sana kuendeleza yale yaliyofanywa na waasisi wetu kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.