Manispaa ya Kinondoni, Kata ya Makongo kunufaika na barabara yenye urefu wa kilometa 10.15 Katika Miradi ya DMDP awamu mpya.
Hayo yamebainika katika hafla ya wiki ya upandaji miti katika kuelekea madhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika Shule ya Sekondari Changanyikeni iliyopo Kata ya Makongo.
Aidha, Diwani wa Kata hiyo Mhe. Joseph Rwegasira amesema katika kuadhimisha maadhimisho haya ya miaka 60 ya Muungano ni mengi yamefanyika lakini kikubwa ni utatuzi wa changamoto ya miundombinu “ Kata ya Makongo imekua ni miongoni mwa Kata yenye changamoto kubwa ya Miundombinu kwa kipindi kirefu, lakini sasa tunamshukuru Raisi wa Jamhuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani ametukumbuka kupitia mradi huu wa DMDP “ Amesema Rwegasira.
Mhe Rwegasira ameendelea kusema kuwa pamoja na hayo yote wananchi wa Makongo wanapaswa kuwa tayari katika kuyapokea maendeleo.
"Niwaombe wakazi wa Makongo muwe tayari katika kupokea maendeleo, timu ya Wataalamu kutoka TARURA, DMDP na Manispaa wanapita katika Mitaa yote kwa ajili ya kutoa elimu shirikishi kwa wakazi wote wanaoishi pembezoni mwa Barabara ili muweze kufahamu umuhimu wa miradi hii ya maendeleo" aeleza.
Aidha, amemaliza kwa kusema viongozi wanapambana katika kuleta maendeleo na ndio dhamana waliyopewa, hivyo wapo kuhakikisha wananchi wanapata wanachokiamini.
"Niwaambie kabisa viongozi wenu tunapambana katika kuleta maendeleo na ndio dhamana mliotupa,tutasimamia mpate mnachokiamini" amesema.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.