Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Godwin Gondwe, ameziagiza shule zote za binafsi wilayani Kinondoni kuwa na wasindikizaji wa kike ndani ya magari ya kubeba wanafunzi.
Agizo hilo amelitoa leo wakati alipotembelea shule ya Starlight iliyopo Tegeta kufuatia tuhuma za ubakaji zinazowakabili dereva na kondakta wa gari la shule hiyo.
Amesema, "nilishaagiza shule zote ziwe na matron wakati wa kuwafuata na kuwapeleka wanafunzi. Lakini agizo hili wengine hawajalitekeleza."
"Sasa naagiza ndani ya siku tatu kuanzia leo Maafisa Elimu Kata na Maafisa Ustawi wafanye ukaguzi ili kubaini utekelezaji wa agizo hili," alisema Mhe. Gondwe.
Aidha, alisema kuwa tayari watuhumiwa hao wameshakamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa hatua za kisheria.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.