Wajasiliamali na wasindikaji wa vyakula mbalimbali katika Kata ya Mbweni wamepatiwa mafunzo ya lishe ili kuweza kusindika vyakula vyao kwa kuzingatia makundi matano ya chakula.
Mafunzo hayo yametolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika kituo cha Kilimo na Mifugo Malolo.
Akiongea katika mafunzo hayo Afisa Lishe wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Emiliana Daud amesema wajasiriamali wanapaswa kuzingatia makundi matano ya chakula ikiwemo kundi la mboga mboga na matunda pindi wanaposindika vyakula vyao.
"Mara nyingi vyakula hivi vinavyosindikwa vimekuwa vikitumia kundi la aina moja hivyo nichukue fursa hii kuwakumbusha wajasiriamali wote kuacha kutengeneza vyakula vya lishe kwa kutumia nafaka za makundi ya aina moja ya chakula kwani husababisha magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kansa itokanayo na sumu kuvu pamoja na kisukari," amesema Bi. Emiliana.
Kwa upande wake Afisa Kilimo Bw . Juma Lukoo amewataka wakazi hao kutumia Kilimo mjini cha upandaiji wa mboga kwa kutumia mifuko ya plastiki, matairi mabovu, mifuko ya saruji na makopo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.