Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mh Kisare Makori ,kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda, katika ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yahusuyo utaalamu wa Kilimo mjini yanayoendeshwa na wakorea kwa kushirikiana na KOIKA kituoni hapo.
Amesema Mafunzo haya ni kufuatia ushirikiano mzuri uliopo kati ya Dar es salaam na jimbo la Gyeongsangnam nchini Korea, yenye lengo la kubadilishana uzoefu katika sekta ya Kilimo mjini, hasa ikizingatiwa ari ya serikali ya sasa ni kujenga Uchumi wa Kati wa viwanda.
"Ni Jambo jema kuwa na ushirikiano wa kimkakati na nchi zilizopiga hatua kwenye sekta muhimu kama za Kilimo, na kuwa tayari kuachilia utaalam huo kwa nchi zinaoendelea kama ya kwetu, hivyo mafunzo haya yachukuliwe kwa umuhimu mkubwa ,hasa nyie washiriki wa semina hii, na mkawe mabalozi wazuri wa kusambaza utaalamu wa kilimo cha mjini"Amesema Makori.
Naye mratibu wa mafunzo haya kutoka Kinondoni Ndg Hija Salehe ambaye pia ni Afisa Kilimo wa Manispaa hiyo amesema, wako tayari kupokea utaalam utakaoleta tija ya Maendeleo katika eneo hili la kilimo, kwani ndio njia pekee ya kumkwamua mkulima kutoka hatua ya chini kwenda ya kati kwa kutumia eneo dogo kupata mazao bora kuelekea uchumi wa kati wa viwanda.
Aidha amezitaja mada zitakazofundishwa kwa siku hizo mbili kuwa ni namna ya bora ya kuongeza ubora wa Kilimo unaoenda sambasamba na hali ya maisha ya mjini, uthibiti wa magonjwa na wadudu katika Kilimo cha mazao ya bustani, mbinu za utunzaji na uendeshaji katika kilimo na mazao ya bustani, pamoja na mpango mkakati wa matumizi sahihi ya mbinu za Kilimo cha mbogamboga.
Akielezea umuhimu wa mafunzo haya kwa Tanzania, Mkurugenzi wa Mahusiano ya kibiashara ya kimataifa kutoka Korea ya Kusini Bw. Youngjun Kwack amesema, wako tayari kusaidiana na nchi ya Tanzania katika kuhakikisha mabadiliko makubwa yanapatikana katika sekta ya Kilimo, kwani hali ya Kilimo iliyoko sasa Nchini, yafanana na miaka ya 70 ya Kilimo nchini kwao.
Mafunzo haya yamehusisha maafisa kilimo wa Halmashauri zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam, wakufunzi kutoka Korea, washiriki kutoka KOIKA, pamoja na wakulima wadogo wadogo wa Kilimo cha mbogamboga kutoka Kinondoni.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.