Zaidi ya Walimu 600 katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Januari 10, 2024 wameanza mafunzo kuhusu mtaala mpya wa elimu ulioanza kutumika hivi karibuni.
Akifungua mafunzo hayo katika ukumbi wa shule ya msingi Kinondoni, Afisa elimu awali na msingi Bi. Theresia Kyara, alisema mafunzo hayo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mwalimu Kyara alisema, "mnamo mwaka 2021 Mheshimiwa Rais baada ya kupitia mtaala wa masomo, alielekeza mtaala huo kufanyiwa maboresho ili uweze kuwapatia wanafunzi ujuzi wa kujitegemea."
Kufuatia maelekezo hayo, Mwl. Kyara alieleza kuwa Manispaa ya Kinondoni imeanza utekelezaji kwa kutoa mafunzo kwa Walimu wanaofundisha Madarasa ya Awali na Msingi ili waweze kutekeleza kwa ufasaha mtaala huo. "Tunataka ifikapo mwaka 2027 malengo ya mtaala huo yatimie kwa asilimia 100," alisema.
Utekelezaji wa mtaala huu utawawezesha Wanafunzi kujifunza kwa vitendo hatua muhimu katika kuboresha mfumo wa elimu na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujitengemea.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Changanyikeni, Everine Ndibalema, pamoja na kuishukuru Serikali kwa kutoa mafunzo hayo, alieleza kuwa wanafunzi watajifunza kwa vitendo jambo litakalowasaidia kujitegemea.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.