Maafisa maendeleo ya jamii 25 kutoka Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya Kiserikali PAKACHA wamefanya ziara kutembelea eneo la viwanda vidogo SIDO Vingunguti kwa lengo la kujionea mashine mbalimbli zinazozalishwa na SIDO ambapo Manispaa inaweza kukopesha kupitia mfumo ya kuwezesha Wananchi kiuchumi.
Akiongea wakati wa ziara hiyo, mratibu wa mradi kutoka Taasisi ya Pakacha Bw. Haruni Jongo amesema wameamua kuwezesha ziara hiyo kwa sekta hiyo kwani wanaamini kwamba wakipata uelewa mpana juu ya bidhaa zinazopatikana hapa nchini watakuwa mabalozi wazuri kwa wanufaika mikopo
Naye Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi Halima kahema alipokuwa akizungumza ameishukuru Taasisi ya pakacha kwa kuwezesha Maafisa kutembelea SIDO, kwani wamekutana na teknolojia mpya ambazo wajasiriamali wanaweza kutumia na kuleta tija katika uzalishaji wa bidhaa zao.
Amesema kwa kutoa mikopo ya vitendea kazi itasaidia wanufaika hao kutumia mikopo yao kwa Lengo husika na kuwataka Maafisa Maendeleo kutumia uelewa walioupata kiwandani hapo kuwahamasisha vijana, walemavu na wanawake wanaotaka mikopo ya kununua vifaa kuwapa elimu sahihi ya vifaa na mahali vinapopatikana.
Kinondoni kwa mwaka wa fedha unaoisha Ilitenga kiasi cha Tsh Bil 3.4 kwaajili ya mikopo ya vijana, wanawake na walemavu ambapo vikundi mbalimbali vinaendelea kunufaika na mikopo hiyo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.