Wanachama wa Chama cha Madalali Mahakama pamoja na Wanadishaji Tanzania wameomba kuanzishwa kanzidata (Database) ambayo itahifadhi taarifa za madalali wote wa Mahakama pamoja na Wanadishaji wote Tanzania ikiwa ni pamoja kuepuka migogoro ya ardhi.
Hayo yamesemwa Machi 04, 2024 na Wenyeviti wa Vyama hivyo kwenye kikao kati ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni pamoja na Wanachama wa Chama cha Udalali na Unadishaji Tanzania katika Ukumbi wa Maafisa wa Polisi "Police Officers Mess" Oysterbay.
Wakiwakilisha Wanachama wote wa Madalali wa Mahakama pamoja na Wanadishaji wametoa wito wao kwa serikali ili kuanzishwe kanzidata ambayo itatatua changamoto za migogoro ya ardhi, ukiukwaji wa sheria, uvunjifu amani pamoja na kuikosesha Serikali mapato.
Mwenyekiti wa TACA, ambacho ni chama cha Madalali na Wanadishaji, alisema "Madalali wasiosajiliwa ni chanzo cha migogoro ya Ardhi," na kuongeza kuwa "uwepo wa kanzidata (Database) utasaidia kujulikana kwa Madalali na Wanadishaji jambo litakalosaidia kuimarisha mahusiano na utendaji kazi kwa kufuata Sheria."
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.