NI KAULI YAKE SULEIMAN JAFO WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI TAMISEMI KUFUATIA UFAULU WA ASILIMIA 93.3%MATOKEO YA DARASA LA SABA KITAIFA 2017
Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa kuongoza katika ufaulu wa asilimia 93.3% wa matokeo ya darasa la Saba Kitaifa kwa mwaka 2017
Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mh Suleiman Jafo alipokuwa akiongea na waalimu pamoja na wazazi wa shule ya Msingi oysterbay hafla iliyofanyika katika ukumbi wa shule hiyo.
Amesema kuwa ufaulu huo ni zawadi tosha kwake yeye kama msimamizi wa shule zote katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na ni kutokana na Juhudi na ushirikiano katika kutekeleza azma ya malengo waliojiwekea
"Mimi ninaspecial message kwa shule hii ya Oysterbay lakini kwa Manispaa nzima ya Kinondoni, Naomba nitoe neno langu la Shukrani sana kwamba kwa zawadi kubwa mlionipa kuanzia Jana nikiwa msimamizi wa shule zote katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Manispaa ya Kinondoni na shule zake ndio wamekuwa wa kwanza ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. "Amesema Jafo.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Aron Kagurumjuli amewapongeza waalimu pamoja na wanafunzi wahitimu wa darasa la saba mwaka huu wa 2017 kwa juhudi kubwa walioifanya kuhakikisha shule za Kinondoni zinafanya vizuri katika ufaulu.
Amesema ni kutokana na maarifa, utashi na weledi wa waalimu kwa kufanya kazi kwa pamoja kwa kushirikiana na uongozi mzima kuhakikisha mwanafunzi anapata kile anachostahili na kwa wakati
"Swala la ufaulu wa mtihani wa darasa la saba kwa Manispaa ya Kinondoni imetokana na juhudi zetu za kazi, juhudi binafsi za kazi, na moyo wa waalimu wetu kufanya kazi kujitolea kufundisha mpaka masaa ya ziada ,kutoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi, ndicho kilichotufanya Manispaa ya Kinondoni kuibuka kidedea " Amebainisha Kagurumjuli.
Katika hatua nyingine Afisa Elimu Msingi wa Manispaa hiyo Bw. Kiduma Mageni amezitaja idadi ya shule zilizofanya mtihani wa darasa la Saba kuwa ni shule 135, kati ya hizo za Serikali ni 76, na 59 ni shule za binafsi.
Amesema kwa Kinondoni wanafunzi waliofanya mtihani huo jumla yake ni 11,721, na imepata ufaulu wa asilimia 93.3%, kitakachopelekea wanafunzi wengi kwenda Sekondari.
Hongera uongozi mzima, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Afisa Elimu, Wakuu wa Shule, pamoja na Menejimenti timu kwa kufanya kazi kwa ushirikiano, na wanafunzi kwa ufaulu mzuri wa matokeo ya darasa la Saba 2017.
Hii ni kuonyesha uongozi uliotukuka, wa kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana ili kufikia lengo na kutekeleza azma na mikakati mliyojiwekea.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.