Kiwango Cha Maambukizi ya virusi vya UKIMWI katika Manispaa ya Kinondoni, kimepungua hadi asilimia 4.7 kwa mwaka 2022.
Hayo yamesemwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Jospeh Rwegasira, wakati akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI iliyoadhimishwa leo katika Kata ya Makumbusho.
Amesema, "Katika kiwango hiki wanaoathirika zaidi ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24." Alitoa wito kuwa, "hali hii (ya kupungua kwa Maambukizi) isitufanye tubweteke bali kuendekeza mapambano huku tukijua kuwa Kinondoni bila UKIMWI inawezekana."
Aidha, alisema kuwa pamoja na huduma zinazotolewa na Manispaa zikiwemo za upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI, alisema kuwa, "huduma hizi bado hazijakidhi kiwango cha uhitaji wa watu kutokana na uhaba wa raslimali." Alisema kuwa, "kwa sehemu kubwa tumekuwa tukitegea wafadhili ambao hutoa asilimia 60 ya bajeti ya UKIMWI."
Hata hivyo alitoa wito kutegemea raslimali za ndani badala ya kutegemea wafadhili ili kutatua matatizo yetu ya ndani. Alitoa wito kwa wadau kuendekeza ushirikiano baina ya Asasi na Kamati za Kata na Mitaa za kudhibiti UKIMWI katika Mapambano dhidi ya Maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Maadhimisho haya yameshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo SMAUJATA, TOKIUKI, TAPOT, HOT, TAWIDO, LHRO, STEPS na wengineo.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini: Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.