NI KAULI YAKE MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH ALLI HAPI ALIPOKUTANA NA WAJASIRIAMALI KUZUNGUMNZIA FURSA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI.
Maafisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kinondoni, wametakiwa kuhakikisha wanatumia maarifa, ujuzi, hekima pamoja na elimu katika kuwasaidia wanachi kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili hasa maswala yahusuyo mikopo,uundwaji wa vikundi na usajili wake.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh Alli Hapi alipokutana na wajasiriamali zaidi ya 2000, kuzungumnzia fursa na changamoto zinazowakabili,katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa King Solomon.
Amesema Maendeleo ya Jamii ndio idara yenye jukumu kubwa la kuhakikisha inasimamia uanzishwaji na uundwaji wa vikundi vya wajasiriamali, inasimamia usajili wake,pamoja na kuwapatia mikopo kwa kufuata Sera na miongozo mbalimbali inayotolewa, ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa Afisa Maendeleo ya Jamii anatakiwa kujua kwa idadi aina ya vikundi vilivyopo kwenye kata yake, zikiwemo changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anapambana kwa vikundi hivyo kupatiwa mikopo.
"Haiwezekani Afisa Maendeleo ya jamii hana majibu ya Kata yake, hawezi kupambana wapate mikopo, hajui vikundi vya vijana wake, hajawahi kuwatembelea, alafu anajiita Afisa Maendeleo, mtu huyo hafai katika Wilaya yangu "Amesema Hapi.
Aidha amewataka Maafisa hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi, na kuhakikisha wanatoa na kuisimamia mikopo kwa walengwa na sio ndugu, jamaa wala marafiki zao.
Mkutano huu wa wajasiriamali uliofanyika leo umeambatana na kauli mbiu isemayo "Uthubutu, ubunifu na Kujiamini "ndio nguzo ya kujikwamua na umaskini.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.