Hayo yamethibitika leo wakati Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mstahiki Meya Sitta, alipokuwa akitoa zawadi kwa wanafunzi washindi wa masomo yaliyoshindanishwa, na kupata alama za juu kwa shule za serikali na zile za binafsi, kuanzia darasa la tatu hadi la sita kwa masomo ya sayansi, hisabati, stadi za kazi na uandishi katika maadhimisho yaliyofanyika leo ukumbi wa oysterbay shule ya msingi
Amesema, kwa kushirikiana na waalimu kufundisha kwa vitendo katika masomo haya ya msingi, ni jambo zuri lenye kuleta ushindani na kuibua vipaji kwa vijana wetu, kunakoenda sambamba na uelewa, pamoja na ufaulu wa masomo hayo, hali itakayopelekea kupatikana kwa wataalamu wazuri watakaoendesha viwanda vyetu, kuelekea uchumi wa Kati wa viwanda.
"Bila kuwa na elimu bora, ndoto yetu ya uchumi wa kati wa viwanda haitakamilika, kwani ndiko watokako wataalam wazuri, hasa Wale wanaosoma kwa vitendo, sasa bila ninyi waalimu pia kuwashika mkono watoto hawa, uchumi wa kati wa viwanda hautafikiwa,"Amesisitiza Meya.
Aidha ameongeza kuwa, kupitia maadhimisho haya ya elimu tunapata faida nyingi ikiwemo: kukuza stadi za kusoma, kukuza vipaji vya wanafunzi, kuongeza ushindani kitaaluma, na kuimarisha ushirikiano na umoja miongoni mwetu.
Nyingine ni kuwahimiza wazazi, waalimu, Jamii na serikali kuongeza ufanisi katika majukumu yao, kuonesha hatua mbalimbali zilizofikiwa katika nyanja za ufundishaji, pamoja na kutoa tuzo mbalimbali kwa washiriki na washindi wa kitaaluma.
Naye Afisa elimu Msingi Manispaa hiyo ndugu Kiduma Mageni amesema, maadhimisho haya ni kwa ajili ya kuakisi, na kufanya tathmini ya kielimu katika masuala husika yaliyopaswa, yanayopaswa na yatakayopaswa kufanyika, ili kufikia malengo chanya kuelekea uchumi wa kati wa viwanda, kwa kuzalisha wataalam wazuri kwenye masomo ya sayansi, waweze kutuendeshea viwanda vyetu.
Katika hatua nyingine Mstahiki Meya huyo ameishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Technolojia pamoja na ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kutoa maelezo sahihi na usimamiaji wa utoaji bora wa elimu, pamoja na program ya LANES kwa ufadhili wa mashindano hayo.
Maadhimisho haya yameenda sambasamba na burudani za muziki, uimbaji wa kwaya na maonesho ya stadi za kazi kutoka kwa wanafunzi 48 walioshindanishwa na kufikia washindi 8 watakaoshiriki maadhimisho hayo ya elimu kimkoa.
Imeandaliwa na
Kitengo cha habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.