Mwenyekiti wa SUMAUJATA, Bi. Leah Makundile, ameitaka jamii kukomesha lugha za matusi kwa watoto wawapo Shuleni na Majumbani ili kutowaharibu akili za watoto.
Bi. Makundile aliyasema hayo wakati wa kikao kazi cha kujadili hatua za kukomesha ukatili kwa watoto ndani ya Manispaa ya Kinondoni Juni 14, 2024. Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini, Kamati ya Usalama Wilaya na wadau.
Aidha, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Mheshimiwa Jackline Rugemalila, alieleza kuwa Mahakama itaendelea kuendelea kupokea mashauri na kupinga matukio ya ukatili yanayoathiri jamii. "Tutaendelea kuwa bega kwa bega katika kuzuia na kuhakikisha hali inakuwa sawa kwa kupinga mmomonyoko wa maadili."
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.