Na Aquilinus Shiduki:
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Hanifa Suleiman Hamza leo amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuleta Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi "Land Tenure Improvement Project" (LTIP) wenye lengo la kuwezesha usalama wa ardhi kwa Watanzania wote.
Bi. Hanifa alitoa shukrani hizo wakati wa kuutambulisha rasmi mradi huo katika ngazi za Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo alisema “utatatua changamoto nyingi za Urasimishaji ndani ya Manispaa.”
Mtaalam Muwakilishi wa Mradi huo kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Aisha Masanja, alielezea kuwa, “kupitia Ardhi Kliniki katika ngazi za Mitaa, mradi utaanza kwa kutoa hati papo hapo, kumalizia kazi za upangaji na upimaji ardhi zilizokwama awamu ya kwanza kupitia Mpango wa Ukwamuaji Urasimishaji Mkoa wa Dar es Salaam.” Bi. Aisha aliongeza kuwa mradi huo utajenga uelewa wa pamoja ili kutekeleza vyema mpango wa ukwamuaji urasimiashaji kwa Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.