Katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka, Madiwani viti Maalumu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na UWT imeadhimisha siku hii kwa kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa Wanawake waliojifungua.
Tukio hilo lifanyika Machi 4, 2024 katika Vituo vya Afya vya Kawe, Bunju na Kijitonyama.
Akiongea na Wazazi katika Vituo hivyo vya Afya, Diwani Viti Maalumu Kata ya Wazo, Mheshimiwa Grace Mkumbwa alisema kuwa, "Kupitia kauli mbiu ya siku ya Wanawake Duniani tumeona isipite bure tumshike mwanamke kwa kufanya shughuli hizi za kijamii."
Aidha, Mheshimiwa Mkumbwa alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuboresha huduma za afya kwa Mama na Mtoto ikiwa ni pamoja na kuboresha vituo hivyo, jambo ambalo limekua msaada mkubwa kwa wanawake wengi.
Kwa upande mwingine pia alimshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Hanifa Suleiman Hamza na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Saad Mtambule kwa ushirikiano mkubwa.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.