Katika kuelekea maadhimisho ya siku Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na WISE Foundation imezindua rasmi kampeni ya upandaji miti ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
Kampeni hiyo imezinduliwa Februari 29, 2024 katika Shule ya Msingi Ally Happy iliyopo Kata ya Bunju, Manispaa ya Kinondoni.
Akiongea kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Suleiman Jaffo, Bw. Anorld Mapinduzi Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Temeke Bw. Anold Mapinduzi amesisitiza upandaji miti kwa wingi ili kutunza mazingira.
“Niwapongeze sana Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na WISE Foundation kwa uzinduzi huu wa kampeni ya upandaji miti ikiwa ni shamrashamra za kuelekea katika maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo huazimishwa kila mwaka ifikapo tarehe Aprili 26, hivyo niwaombe walimu wote wahimize wanafunzi katika utunzaji wa mazingira yetu,” amesema Bw. Mapinduzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa WISE Foundation Bi. Dorca Mwanji amesema kuwa katika kampeni hiyo wanatarajia kupanda miti zaidi ya 2,000 katika Wilaya ya Kinondoni hasa katika maeneo ya shule.
“Tukiwa tunaadhimisha siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sisi kama Taasisi ya WISE tumejipanga kupanda miti zadi ya 2,000 ikiwa leo tumeanza kwa kugawa miti zaidi ya 300 katika shule mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni,” amesema Bi. Dorica.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.