NI KUHUSIANA NA UTAALAMU ADIMU NA WA KISASA WA JINSI YA? KUZALISHA MALISHO YA HYDROPHONIC .
Kuelekea kilele cha Nane nane Mkoani Morogoro Manispaa ya Kinondoni imejipanga vema katika maswala ya Ufugaji.
Leo inakuletea Technolojia ya kitu kinaitwa Hydrophonic Fodder.
Technolojia hii ya Hydrophonic fodder ni mbinu ya kukuza mimea kwa kutumia mchanganyiko wa vurutubisho vya madini katika maji bila kutumia udongo.
Mchakato huu huchukua muda wa siku 5-7 kukamilika. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua Kilo moja ya mbegu za ngano au mtama au shayiri au mahindi na kuziotesha kisha kumwagiliwa virutubisho maalum(Hydrophonic Nutrients).
FAIDA ZA CHAKULA CHA HYDROPHONIC FODDER KWA MIFUGO.
Ni nafuu sana ukilinganisha na gharama za chakula cha madukani.
Kina virutubisho na vitàmini mara 3 zaidi ya chakula cha kawaida.
Hupunguza magonjwa ya mfumo wa hewa kama vile mafua kwa mifugo na mfugaji kwani hakina vumbi.
Kina Protein ya kutosha, chakula chake ni laini, mifugo hukua kwa haraka Sana na hupunguza gharama za ufugaji kwenye manunuzi ya chakula kwa asilimia 50-75.
HATUA KATIKA KUZALISHA HYDROPHONIC.
Mfugaji anaweza kuzalisha malisho yake mwenyewe nyumbani. Mambo muhimu ya kufuata ni haya hapa :
Chagua mbegu ambazo hazijaanza kuchipua, na hazina kemikali ama dawa ya aina yeyote.
Loweka mbegu katika mchanganyiko wa maji na chlorine kwa masaa mawili kuepusha kuvunda, ama vimelea vya magonjwa kumea na kukua kwenye malisho.
Zitoe mbegu kwenye maji, kisha zioshe, ziloweke kwenye maji safi kwa masaa 24 kuwezesha mbegu kufyonza maji vema.
Katika kupanda mbegu, pima kilo mbili za mbegu kwa kila trei yenye urefu wa cm 80 kwa upana wa cm 40.
Sambaza mbegu kwenye trei kwa usawa, (zisizidi cm 3kimo) ili kuwe na nafasi ya kutosha kwa kila mbegu kuchipua.
Hakikisha trei zinamatundu kwenye kitako(chini) ambayo yamesambaa kwa usawa kuwezesha maji ya ziada kutoka.
Hamishia trei kwenye chanja ulizotengeneza. Mbegu zitaanza kuota katika hatua hii. Fanya hii ni siku ya kwanza.
JINSI YA KULISHA.
KUKU: kwa kuku 100 wanaotaga (Layer) wape kilo 8 za hydrophonic na waongezee kilo 4 za chakula cha layer.(Layer Mash) kwa siku.
Nguruwe: Katika unenepeshaji wake kilo 2 za hydrophonic na 1.5 za chakula kikavu (Nafaka) kwa nguruwe mmoja kwa siku.
Ngombe, Mbuzi :wanaweza kutegemea majani haya tu na kuwa na uzalishaji mzuri bila nyongeza ya mchanganyiko wa nafaka.
Sungura :wanaweza kutegemea majani haya tu lakini ni vema kuwapa nyongeza ya mchanganyiko.
Kwa elimu zaidi juu ya technolojia ya Hydrophonic, usikose kutembelea banda la Manispaa ya Kinondoni ukutane na wataalamu wa Mifugo wapate kukujuza mengi zaidi.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.