Hayo yamedhihirika pale ambapo umati wa watu, wakiwemo viongozi wa vyama na Serikali wakimiminika kwa lengo la kujionea na kujifunza utaalam wa ufugaji, uvuvi pamoja na kilimo cha faida kuelekea utekelezaji wa kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "Wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa ajili ya maendeleo ya viwanda
Uvutiaji wa banda hilo umetokana na bidhaa zilizomo ndani yake,aina ya kilimo na ufugaji unaozingatia ubora na faida, wakiwemo wataalam mbalimbali wenye kutoa elimu na maarifa ya jinsi ya kufikia malengo yanayotakiwa katika sekta hiyo ya kilimo na mifugo.
Kadhalika katika banda hili pia utakutatana na wataalam pamoja na wadau wenye utayari wa kutoa elimu kuhusiana na umuhimu wa matumizi ya mnyororo wa thamani katika matumizi ya pembejeo bora za Kilimo, mifugo na uvuvi.
Tembelea banda la Kinondoni uhabarike, uelimike kuhusiana na sekta hii muhimu, kuelekea uchumi wa kati wa viwanda ikiwa ni pamoja na kuunga mkono bidhaa za wajasiriamali waliowezeshwa kielimu, na kupatiwa utaalam pamoja na mbinu mbalimbali za ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.