Katika kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Manispaa ya Kinondoni wahamasisha utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti 500 katika Kata ya Makongo Juu.
Akiongea katika zoezi hilo la upandaji miti ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya utunzaji wa mazingira yaliyofanyika leo Aprili 23, 2024 katika Shule ya Sekondari Changanyikeni, Afisa mazingira kutoka NEMC Bw. Eston Waria amesema.
"Miti ina faida nyingi ikiwepo upatikanaji wa hewa ya oksijeni, lakini pia inaondoa hewa ya ukaa itokanayo na shughuli mbalimbali za kijamii, pia inasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza joto na hali ya ukame inayotokana na mabadiliko ya tabia nchi, hivyo yatupasa kutunza mazingira yetu kwa kupanda miti ya kutosha kwenye maeneo yetu,".
Aidha Bw. Waria amesema kuwa kumekua na changamoto mbalimbali ambazo tumekutana nazo katika mazingira ikiwemo utiririshaji wa maji taka katika maeneo mbalimbali hasa kipindi hiki cha mvua, wengi wamekua wakitumia wakati huu wa mvua kufungulia vyoo vyao jambo ambalo ni hatari kwa afya hivyo niwaombe tuendele kukumbushana umuhimu wa utunzaji wa mazingira yetu
Sambamba na hayo pia Bw. Waria amewataka Wakazi hao kutotupa taka kwenye mitaro na kwenye vyanzo vya maji ambapo inapelekea kuziba kwa baadhi ya mitaro na kusababisha mafuriko kwa baadhi ya maeneo hivyo tuzingatie hayo ili kuepukana na mafuriko hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.