Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 Bw. Godfrey Mnzava ameridhishwa na Kongamano la Vijana 949 wa Manispaa ya Kinondoni lililofanyika katika Mkesha wa Mwenge katika Viwanja vya Bunju A. Bw. Mnzava aliyabainisha hayo Mei 11, 2024 baada ya kumaliza kukagua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi 8 iliyotekelezwa na Manispaa ya Kinondoni. Kadhalika, Bw. Mnzava alipongeza kongamano hilo lililokuwa na adhima ya kuwakusanya vijana katika kufikia malengo ambayo yalisaidia vijana kujua historia ya nchi, kujua falsafa ya Mwenge na fursa zilizopo na kuzichukua kwa vitendo.
" Kinondoni imefanikiwa kuzungumza na vijana wengi hivyo ipo kiu na sababu ya kuendelea kuwakutanisha Vijana na Viongozi ili kupata wasaa mzuri wa kujadili, kupata mawazo na kujua mipango yao". Amesema, Bw. Mnzava. Vile vile, aliitaka Manispaa ya Kinondoni kutoa elimu, hamasa na maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
"Ikiwa kuna vituo 1,630 vya Uchaguzi, Wadau na Viongozi wa Chama washughulikie hatua mbalimbali za Uchaguzi". Ameongeza Bw. Mnzava.
Aidha, Mgeni Maalum wa Mdahalo huo Bw. Richard Kasesela aliwataka vijana kutambua ya kuwa ili kufikia malengo yao ni lazima wajiamini, wawe na malengo, nidhamu, uaminifu, uwajibikaji, utu, utiifu na upendo.
Miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na fursa mbalimbali za kiuchumi, elimu ya uzalendo, uadilifu, stadi za maisha, uongozi elimu ya kupinga na kupambana na kuzuia rushwa.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.