Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani Septemba 29, 2024, Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Hospitali ya Muhimbili (JKCI) wamezindua zoezi la upimaji wa moyo kwa Watoto wa Shule za Msingi.
Zoezi hilo lenye lengo la kuwafikia Watoto zaidi ya 2,000 limezinduliwa Agosti 23, 2024 katika viunga vya Shule ya Msingi Hananasifu.
Kwa upande wake, Mratibu wa Tiba ya Magonjwa yasiyoambukizwa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Omary Mwangaza amesema kuwa, Magonjwa yasiyoambukizwa kama vile Moyo yamekuwa na athari sana kwa Jamii nyingi kutokana na gharama zake.
Aidha, katika Shule ya Msingi Hananasifu jumla ya Watoto 684 wamefanyiwa vipimo vya Moyo, kati yao 3 wamekutwa na tatizo la Matundu katika moyo ambapo 2 watafanyiwa matibabu bure pia Wazazi/Walezi wao watapatiwa Hela za kujikimu wakati Watoto hao wanapatiwa huduma, huku mmoja ataendelea kufuatiliwa kwa ukaribu zaidi kwakuwa hajakutwa na tatizo kubwa kama wenzake.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.