Akizindua zoezi hilo kwa majimbo yake mawili ya uchaguzi, Mkuu wa Wilaya ya hiyo Mhe. Godwin Gondwe amesema uzinduzi huu ni katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan la kutaka utambuzi na uainishaji wa maeneo kwa majina na namba, hali itakayoleta tija kwa Taifa letu.
Amesema "Tumewatengenezea wananchi mfumo wa kuweza kuwafungulia uchumi wa kidigitali, kwa sababu sasa hivi kama mtu anafanya biashara yake mtandaoni, anaweza akapiga picha na kusema kuwa biashara yake iko wapi, lakini pia inamsaidia katika masuala ya usalama" Amesema Gondwe.
Ameongeza kuwa anwani za makazi pia ni maandalizi ya kuelekea kwenye sensa inayotarajiwa kufanyika tarehe 22 mwezi Agosti, mwaka huu, hali itakayorahisisha katika kufanikisha kwake .
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Songoro Mnyonge katika kuunga mkono azma ya uwekaji wa anwani za makazi kwa wananchi wake amesema jambo hili linapaswa kutekelezwa kwa ufanisi na umakini ili liweze kufikiwa lengo lililokusudiwa.
Akitoa ufafanuzi wa hatua za awali ambazo Kinondoni imechukua mpaka sasa katika kufanikisha zoezi hili la anwani za makazi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Hanifa Suleiman amesema Manispaa ya Kinondoni imeshakamilisha andiko pamoja na masuala ya bajeti ambayo ndio msingi mzima wa utekelezaji na ukamilishwaji wa jambo hili na kuwataka wana Kinondoni wote kutoa ushirikiano ili likamilike kwa wakati.
Uzinduzi huo pia umehudhuriwa na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe Kheri Misinga, Watendaji wa Kata na Mitaa, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wote pamoja na wananchi.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.