Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Saad Mtambule, Februari 03, 2024 amezindua zoezi la ugawaji hati miliki ya ardhi (Ardhi Clinic) katika Manispaa ya Kinondoni.
Uzinduzi huo ulifanyika mapema katika Kata ya Wazo ambapo wananchi walifika kwa ajili ya utatuzi wa changamoto za ardhi pamoja na kupatiwa hati ya ardhi papo kwa papo.
"Hii ni fursa adhimu kwa wakazi wa Kinondoni kwani Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanzisha Ardhi Clinic ili kutatua changamoto za migogoro ya ardhi kwa kutoa hati miliki kwa wanaomiliki ardhi". Alisema Mhe. Mtambule.
Aidha, Mhe. Mtambule aliwataka viongozi kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kufika katika Stop Centres ili kuweza kupata Hati miliki za Ardhi."
Niwaombe sana akina mama mjitokeze katika fursa hii kwani akina mama na watoto ndio wahanga wakubwa wa migogoro ya ardhi". Aliongeza, Mhe. Mtambule.
Vile vile, Mhe. Mtambule aliwataka wananchi kuacha kuchochea migogoro ya ardhi kwa kuepuka kununua maeneo yasiyopimwa.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, alisema, "Tumepokea mpango huu kwa mikono miwili, hii itatoa picha halisi ya kuhusiana na migogoro ya ardhi iliyopo hivyo itasaidia kujua namna ya kuweza kutatua migogoro hiyo".
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.