Kinondoni imetoa onyo kali kwa watu wanaouza wanyama jamii ya mbwa na Paka kiholela kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya ufugaji mjini.
Onyo hilo limetolewa leo na katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi Stella Msofe, alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kichaa Cha mbwa Duniani yenye kaulimbiu isemayo "TOKOMEZA KICHAA CHA MBWA: TUSHIRIKIANE, KUCHANJA" na kuzindua rasmi chanjo ya ugonjwa wa kichwa cha mbwa hafla iliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packer's.
Amesema sheria hairuhusu mbwa na paka kupangwa barabarani na kuuzwa, wanyama hawa Wana haki zao na kuna maeneo maalum ambayo biashara hii inatakiwa kufanyika, hivyo Wananchi wafuate sheria ili kwa pamoja tuweze kutokomeza magonjwa yanayozeza kutoka kwao wanyama na kuja kwa binaadamu ukiwemo huu wa Kichaa cha mbwa.
"Napenda kutumia maadhimisho ya siku hii kuwakumbusha wenzetu wanaoishi na mifugo majumbani mwao kufuata sheria za ufugaji mjini ili kudhibiti mbwa wanaozurura na Wananchi waache mara moja biashara ya kuuza mbwa barabarani"
Ameongeza Bi Msofe.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya mifugo na uvuvi Manispaa ya Kinondoni Bi Patricia Henjewele amesema ugonjwa wa kichwa cha mbwa unaowapata mbwa pia unawapata binaadamu, na ni vigumu kutibu binaadamu ambae anakuwa ameambukizwa ugonjwa huu hivyo ni bora zaidi kuchanja mifugo ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa.
Amesema zoezi la chanjo kwa mbwa na paka ambalo limezinduliwa leo, litakuwa endelevu kwa kipindi cha mwezi mzima katika kata mbalimbali zilizopo wilaya ya Kinondoni hivyo Wananchi wawasiliane na Maafisa mifugo wa kata husika.
Aidha amewashukuru Taasisi ya Every living Things inayojihusisha na haki za wanyama hususani wanyama wanaozurura mitaani kwa kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kutokomeza ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa.
Siku ya kichaa cha mbwa duniani huadhimishwa kila ifikapo Tar 28 mwezi Septemba ambapo kwa Kinondoni wameadhimisha kwa kutoa chanjo kwa mbwa na paka dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa, Kutibu wanyama watakaogundulika na magonjwa ya aina mbalimbali, Kuogesha wanyama kwa lengo la kuua kupe na viroboto na kukata kucha zilizodidi.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.