Kinondoni kupitia kitengo cha Ustawi wa jamii kimeendesha mafunzo kwa maafisa ustawi 73 yanayohusu kuwajengea uwezo, ikiwa ni pamoja na kusimamia misingi na weledi unaoenda sambamba na usimamizi wa Sheria katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa DMDP, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dkt Samwel Laizer amesema kuwa mafunzo hayo Ni msingi madhubuti utakaowaongoza katika kutekeleza majukumu yao katika Kata 20 za Halmashauri yetu ikiwa ni pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.
Amesema kazi ya ustawi wa jamii inahitaji weledi na uvumilivu wa hali ya juu kwani ni kazi ambayo muhusika hukutana na makundi mbalimbali ya watu ambapo wengi wao wanakuwa wanapitia changamoto tofauti za maisha.
"Hii kazi inahitaji kujitolea, wakati mwingine ni kazi ya wito, mtakapokutana na changamoto mbalimbali kwenye kutimiza majukumu yenu tutakuwa pale kuwasaidia ili nanyi muweze kupata kitu Cha kujifunza"
Naye Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Kinondoni, Bi Judith Kimaro alipozungumza amesisitiza umakini na usikivu katika kuzingatia matumizi ya lugha wakati wa kutimiza majukumu yao kwani watakutana na makundi mbalimbali ya wahitaji huku akiwataka kuibua watoto wenye ulemavu wanaofichwa majumbani kwa dhana na Imani potofu, ili waweze kupatiwa haki zao za msingi.
Aidha amewataka kuzingatia suala la mavazi yenye staha, kwani ndio msingi imara wa utekelezaji wa majukumu yao unaoenda sambamba na nidhamu makazini, utakaorahisisha uwajibikaji katika sekta hiyo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha habari na uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.