Baraza hilo lenye wajumbe saba akiwemo Mwenyekiti na msaidizi, Katibu na Msaidizi wake, mtunza fedha na wawakilishi wawili, limeundwa kwa uchaguzi uliofanyika kwa wazee wawakilishi kutoka kata 20, za Manispaa hiyo kupiga kura katika kikao kilichofanyika katika moja ya kumbi za Kanisa katoliki Manzese.
Akiongoza zoezi hilo, kwa niaba ya Maganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Bi Nusura Kessy amesema, wazee ni hazina ya Taifa, hivyo yapaswa kupaza sauti juu ya maswala yanayowahusu na kuwasemea haki zao za Msingi pale inapobidi ili waweze kutatuliwa.
"Wazee ni hazina ya Taifa, nilazima walindwe, waheshimiwe watunzwe, na mashauri yao yasikilizwe, hivyo kwa baraza hili la wazee wa Wilaya mtakaloliunda kwa kufanya uchaguzi huru na wa haki unaozingatia vigezo leo, mtakuwa mmejitendea haki lakini pia baraza hilo likawe kisemeo katika yale yanayowapasa kusema " Bi. Nusura Kessy.
Awali akitaja majukumu ya baraza hilo la wazee la Wilaya, Bi. Judith Kimaro ambaye pia ni mkuu wa Kitengo cha ustawi wa jamii amesema Baraza linalo majukumu yake ya msingi ambayo ni kupitia majumuisho ya kero za wazee zilizoletwa na wawakilishi, kufanya mkutano wa baraza la wazee la Wilaya kila baada ya miezi mitatu, kuwasilisha kero za wazee kwenye baraza la madiwani, kuchagua wawakilishi wawili kwenye baraza la madiwani, kushawishi Halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya miradi ya uzalishaji ya wazee pamoja na kuratibu mabaraza ya wazee ya Kata.
Naye mratibu wa wazee Manispaa ya Kinondoni Bi Neema Mwalubilo alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya wazee Manispaa ya Kinondoni amesema ni ya kiridhisha kwani wameweza kuunganishwa kwenye huduma za afya kwa kutengenezewa vitambulisho takribani 11,340 vya msamaha .
Aidha ameainisha mikakati iliyopo ya kuinua hali ya wazee katika Manispaa hiyo kuwa ni kuhakikisha wote wanapata kadi za matibabu, kuwaongezea na kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi pamoja na kuwaunganisha na wadau mbalimbali kwa ajili ya misaada.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.