Manispaa ya Kinondoni yatoa semina elekezi ihusuyo Mfumo wa kihasibu na utoaji taarifa za kifedha katika vituo vya kutolea huduma ngazi za chini.
Semina hiyo iliyofunguliwa na Mwekahazina wa Manispaa Bw. Maximillan Tabonwa imefanyika leo katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Manispaa uliopo Magomeni.
Akifungua semina hiyo Maximilian amesema kwa kuwa sasa Serikali inakusudia kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma, Mfumo huu utasaidia kutoa na kutunza taarifa hizo za fedha kwa usahihi na kwa wakati.
Amezitaja faida zitakazopatikana kutoka kwenye mfumo huo kuwa ni Urahisi wa upatikanaji wa taarifa za kifedha ngazi ya chini, kuwa na uwazi katika matumizi, kupunguza gharama za uchapishaji wa vitabu vya matumizi ya Fedha kwa Halmashauri, pamoja na kuwa kumbukumbu nzuri ya kudumu ya matumizi ya fedha kwenye Serikali.
Aidha amewataka wahasibu hao kuwa makini katika kusikiliza, kuelewa, ili kuendana na matakwa ya mfumo huo kwa maswala ya matumizi na utunzaji wa taarifa za kifedha.
Semina hii imehusisha waalimu wakuu wa shule za Msingi na Sekondari, wahasibu wa vituo vya kutolea huduma ngazi za chini ambavyo ni vituo vya Afya, Zahanati pamoja na Hospitali.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.