Kituo cha mafunzo ya kilimo Malolo kilichopo Mabwepande Manispaa ya Kinondoni, leo kimetoa mafunzo yahusuyo uendeshaji wa kilimo cha kisasa mjini unaokidhi viwango kuelekea uchumi wa Kati wa viwanda kwa Baraza la Madiwani Ubungo.
Mafunzo hayo yaliyotolewa na Afisa kilimo wa Manispaa hiyo, Ndugu Salehe Hija, yamelenga kuimarisha sekta ya kilimo cha kisasa, hususani kilimo cha kitalu nyumba kitumikacho mijini, ikiwa ni pamoja na matumizi ya eneo, aina ya uoteshaji wa mbogamboga pamoja na aina ya ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa.
Akishukuru kwa mafunzo hayo, kiongozi wa msafara kutoka Ubungo ambae pia ni diwani wa kata ya kibamba, Mh. Mgawe Stanley amesema Ubungo wako tayari kufuata nyao hizo kwa kuhakikisha sekta hii ya Kilimo inaimarishwa kuelekea uchumi wa Kati wa viwanda.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.