Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imetembelewa na timu ya wataalam wa mfumo wa Planrep kutoka Tamisemi kwa lengo la kuangalia mafunzo yanavyoendelea.
Akizungumnzia ujio wao mmoja wa wataalam hao Bi Beatrice Mungure amesema timu hiyo pia imekuja kwa lengo la kusaidia na kuona jinsi mfumo huo mpya unavyofanya kazi.
Amesema mfumo huo ni shirikishi kwani wakuu wa idara na Maafisa bajeti wa Halmashauri wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja.
Akizitaja faida za mfumo huo mtaalam kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Bw. Athuman Mayunga amesema mfumo wa uandaaji wa bajeti wa serikali kwa sasa utapunguza gharama za uandaaji na uchapishaji wa vitabu vya bajeti, ni mfumo shirikishi hivyo kumfanya mkuu wa idara na Afisa bajeti kuwajibika katika maeneo yao.
Ameongeza kuwa ni mfumo utakaozifanya Halmashauri kufuata ratiba kwa maswala ya uandaaji wa bajeti, na pia kumsaidia kila mshiriki wa uandaaji bajeti kujua majukumu yake.
Akitoa tathmini ya mafunzo hayo ya Planrep kwa Timu hiyo Muwezeshaji wa mafunzo ambaye pia ni Afisa mipango Ndugu Almas Abdi amesema mpaka sasa wakufunzi wamefikia hatua ya kuweza kujua majukumu yao, kuingiza malengo pamoja na kuyapangia matumizi.
Amesema mafunzo haya yatafanyika kwa siku tano, na yamehusisha wakuu wa idara pamoja na Maafisa bajeti kwani mfumo wenyewe unaelekeza hivyo.
Akizitaja changamoto zilizopo Almas amesema kubwa ni swala la upatikanaji wa mtandao unaokidhi mahitaji pamoja na watumiaji wa mfumo kutokuwa rafiki na mfumo wenyewe.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.