ANGALIA NJIWA HAWA!
Sekta ya Mifugo Manispaa ya Kinondoni katika maonesho ya Nane nane ya mwaka 2017 imedhamiria kutekeleza vema kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa Kati".kwa kuwainua wafugaji.
Hii imedhihirika pale ambapo mfugaji, na mjasiriamali Ndg Mustapha Ismail alipotakiwa kuzungumnzia aina ya Njiwa walioonekana kuwa kivutio cha wengi katika maonesho haya.
Amesema njiwa hawa wanajulikana kwa jina la Simba na ni kutokana na muonekano wao wa kuwa na manyoya mengi, na asili yake ni Marekani na Uarabuni.
Amesema ni ndege wenye faida kubwa na mafanikio katika kuongeza kipato kwa mtu yeyote yule na kwa wakati wowote ule mfano njiwa hawa hutotolewa mayai kuanzia siku ya kumi na nne(14) hadi kumi na tano(15). Yai lake moja ni shilingi 30,000/=na kwa mwaka hutotoa mara mbili mpaka mara tatu.
Amezitaja faida nyingine kuwa ni njiwa wanaodumu kwa muda mrefu, na wasiowepesi kushambuliwa na maradhi, pia hutumika kama urembo, na kinyesi chake kama mbolea.
Ameongeza kuwa ukiwa nao ndani ni ulinzi wa kutosha kutokana na sauti ya tofauti na muonekano wa tofauti wanaoukuwa nao wakati wa hatari, na ni chanzo kikubwa cha kipato kwani njiwa mmoja huuzwa tsh 700,000/=
Njiwa hawa aina ya Simba wanalishwa vyakula vya mtama, Choroko, Ngano, Karanga na kunde, na mchanganyo huo wa vyakula unahitaji umakini wa kutosha.
Naye Mtaalamu wa Mifugo kutoka Manispaa ya Kinondoni amesema njiwa hawa ni ndege wa asili na ndio maana wanakula vyakula vya asili.
Ameongeza kuwa hawana gharama kubwa kwenye ulishaji ukilinganisha na ndege wengine mf Kuku ambao wanakula vyakula vya viwandani ambavyo ni gharama.
Njiwa hawa wamekuwa kivutio kikubwa cha watu kutaka kuwaona.
Ni banda la Kinondoni pekee, utakutana na haya na mengine lukuki kuhusiana na mifugo, kilimo na uvuvi.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.