Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetajwa katika orodha ya Halmashauri 9 kati ya Halmashauri 185, zinazofanya vizuri kwa uhuishaji wa tovuti nchi nzima.
Orodha hiyo imetajwa na Waziri wa Habari,utamaduni,sanaa na michezo Mh.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akifungua mkutano Wa 14 wa mwaka wa Maafisa Mawasiliano serikalini unaofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha.
Dkt Mwakyembe amesema kupitia ofisi ya OR-Tamisemi, mwezi wa tatu 2017, ilizindua tovuti za Mikoa pamoja na Halmashauri kwa lengo la kuboresha utoaji wa taarifa kwa Umma ili kuongeza uwazi na uwajibikaji.
"Tulipokuwa tukizindua tovuti hizi mwezi machi 2017,tulisisitiza tovuti hizi kutokuwa magofu bali majokofu ya habari, hivyo tulizizindua tovuti hizo za Mikoa pamoja na Halmashauri ili
Kuongeza uwazi na uwajibikaji "alisema Dkt Mwakyembe .
Amesema tovuti hizo zinatakiwa kuwa na taarifa sahihi na kwa wakati, ili kutoa nafasi kubwa ya watanzania kuzipata na kujua Serikali yao inafanya nini na kwa wakati gani.
Amewataka maafisa habari kuwajibika kwa kutoa taarifa hizo kwani kwa kutokufanya hivyo ni kuwanyima wananchi haki ya kupata taarifa na Utatakiwa kuwajibishwa kwa hilo.
Amezitaja Halmashauri nyingine zilizofanya vizuri kuwa ni Kishapu, Mlele, Ubungo, Ilala, Kibaha, Mtwara Mikindani, na Mufindi.
Mkutano huu unaondelea Mkoani Arusha umehusisha takribani maafisa , mawasilino,habari na uhusiano mia tatu kutoka taasisi mbalimbali za serikali, Wizara, idara za Serikali, sekretarieti za Mikoa pamoja na Halmashauri.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.