Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uongozi Mh. Benjamin Sitta, ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, katika ziara yake aliyoifanya kwa lengo la kukagua na kutathmini thamani ya miradi inayotekelezwa na fedha zilizotumika.
Amesema kwa vituo hivi vya ukataji wa tozo mbalimbali kusogezwa karibu na wananchi kutarahisisha upatikanaji wa huduma utakaopelekea ongezeko la ukusanyaji wa mapato, kadhalika na kupunguza msongamano wa watu usio wa lazima.
"Serikali ya sasa iko kwa ajili ya wananchi, kuzijua changamoto zao,na kuzitatua ,huo ndio msimamo wa Serikali hasa ikilenga swala la matibabu sahihi kwa mama na mtoto, pamoja na ukusanyaji wa mapato unaoenda sambamba na ulipaji wa kodi , hivyo kwa sisi Kinondoni sina budi kusema tunatekeleza tena kwa kiwango cha juu kabisa "Amesema Meya.
Akitoa ufafanuzi wa vituo hivyo vya kutolea huduma ya ukusanyaji mapato na ukataji wa leseni kwa mfumo wa kielektroniki kwa Kamati hiyo, Afisa Tehama kutoka Manispaa Ndg EdgarJereman amesema mpango uliopo ni kuboresha huduma hizi kwa kila Kata, ambapo vituo vilivyofungwa kwa sasa na kufanya kazi ni kilichopo Mwenge Nakiette, Kibo Complex tegeta na Bunju ofisi za Serikali ya Mtaa.
Katika ziara hiyo iliyoambatana na wataalam wamepata fursa yakutembelea kituo cha kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo wa kielektroniki kilichoko Mwenge na kuona jinsi kinavyotoa huduma kwa wanachi wengi na kwa ufanisi mkubwa.
Kadhalika wametembelea mradi wa Ujenzi wa jengo la huduma ya mama na mtoto katika zahanati ya Madale, Kiwanja namba 1024 kilichoko Mwenge na ujenzi wa barabara ya Makanya yenye urefu wa Km 1.5 kwa kiwango cha lami.
Aidha kamati imeshauri, huduma zote za kijamii kusogezwa karibu kwani kwa kufanya hivyo kutarahisisha upatikanaji wake kwa wananchi ambao ndio walengwa wetu inapokuja swala la utoaji na upatikanaji wa huduma hizo bora.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.