NI KWA AJILI YA UJENZI NA MABORESHO YA MTO NG'OMBE NA BARABARA YA SHEKILANGO KWA KIWANGO CHA NJIA NNE.
Akisaini mikataba hiyo, kati yake na makampuni hayo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg. Aron Kagurumjuli amesema, mradi wa mto ng'ombe utakaogharimu bilioni 32, utajengwa na kampuni ya China Henan International Cooperation Group CO. LTD na mradi wa barabara ya shekilango wa njia nne utakaogharimu shilingi 26 bilioni, utajengwa na Kampuni ya China road and bridge Cooperation hali itakayosaidia si tu kuboresha maeneo hayo bali pia kuyapandisha hadhi kwa kiwango kusudiwa.
Amesema katika mikataba hiyo pia yatajengwa mabwawa ya kukusanyia maji eneo la karibu na chuo cha maji kutoka maeneo mbalimbali na maji hayo yataruhusiwa kuingia taratibu mto ng'ombe hali ambayo itasaidia kupunguza mafuriko.
Akishuhudia utilianaji sahihi mikataba hiyo, Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta amesema, Serikali ya awamu ya tano ni Serikali sikivu yenye lengo la kuboresha makazi duni na kuwatoa wananchi kwenye kifungo cha mateso ya mafuriko, na ujenzi huu wa mto ng'ombe utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kadhia hiyo iliyokuwa ikisumbua wananchi wa maeneo ya Tandale na kijitonyama.
Aidha Meya Sitta pia amewataka makandarasi wanaojenga miradi hiyo kujenga kwa wakati na kwa ubora stahiki ili waweze kumaliza kero iliyokuwa inawasumbua wananchi kwa muda mrefu.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.