Pongezi hizo zimekuja Mara baada ya timu ya wataalamu kutoka Mkoa wa Dar es salaam kufanya ziara kutembelea vikundi vya wanufaika wa mikopo hiyo ya asilimia kumi kwa vijana, wanawake na walemavu kwa Manispaa ya Kinondoni.
Kiongozi wa timu hiyo, ambaye pia ni mratibu wa dawati la uwezeshaji wananchi kimkoa Bi. Zubeda Salum Masoud ameongeza kuwa lengo kubwa ni kuangalia vikundi vinavyohusika na uzalishaji na jinsi walivyoitumia mikopo hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa namna gani Serikali inaweza kuwasikiliza, namna wanavyoweza kuuza na kupanua masoko yao.
"Kwa Kinondoni tumetembelea vikundi 8, Tumeviona vikundi vyote utendaji wao unaridhisha na mikopo ambayo wameipata inaendana na kile ambacho wameandika kwenye michanganuo yao, niwapongeze Sana wataalamu kwa Usimamizi mzuri" Ameongeza Bi Zubeda Salum
Aidha ameainisha changamoto kubwa zinazokabili vikundi hivyo kuwa ni uelewa wa wafanyabiashara katika kutafuta masoko ili yaendane na ushindani wa soko, upatikanaji wa Cheti Cha viwango kutoka TBS, hali inayochangia kukosekana kwa masoko kutokana na kutokuwa na vyeti kamili.
Mratibu huyo ameahidi kuwakutanisha wajasiriamali hawa na Taasisi mbalimbali zinazojihusisha na masuala ya kuongeza thamani ya bidhaa ikiwa ni pamoja na TBS, BRELA na kupata leseni za Biashara.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Kinondoni Bi Halima Kahema ameshukuru kwa ujio wa wataalamu hao kwani kutaongeza chachu kwa wajasiriamali kujituma zaidi na kuzingatia ushauri wote wa kitaalamu waliopatiwa ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa mikopo kwa walengwa.
Vikundi vilivyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na vile vinavyojihusisha na kilimo na ufugaji, utengenezaji wa bidhaa za ngozi, usindikaji wa viungo, uzalishaji wa vinywaji baridi pamoja na utengenezaji wa sabuni.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na uhusiano
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.