Pongezi hizo zimetolewa leo na Mwenyekiti wa kamati ya Siasa ya Wilaya Mh Harold Maruma, alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa lengo la kujiridhisha thamani ya fedha inayoenda sambamba na mradi husika.
Amesema Konondoni kwa miradi tuliyopitia, inatia moyo, kwani imetekelezwa kwa ubora na umakini wa hali ya juu, wenye kuleta tija kwa wananchi.
Amesema "dhana ya Halmashauri ni ushirikiano na mashauriano, hasa kunapokuwa na swala la utekelezaji na ukamilishaji wa jambo fulani, hivyo kwa ubora wa miradi hii hasa ule wa zahanati, inaonesha kuwepo na ushirikiano mzuri na mashauriano katika timu wenye maridhiano ambapo kukamilika kwake kutasaidia kutatua changamoto nyingi hasa zile za mrundikano wa wagonjwa katika hospitali moja" Harold Maruma.
Ameongeza kuwa ni lazima watendaji wawe wazalendo katika kuhakikisha miradi hii inaenda sambamba na utekelezaji wa ilani ya Chama Tawala, unaosimamia ubora wa thamani ya fedha iliyokusidiwa na mradi unaotekelezwa ili iweze kuleta tija na manufaa kwa wananchi wetu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo katika kusisitiza ubora wa miradi, amewataka watendaji kuwa wazalendo na wawajibikaji ili kuhakikisha tija inapatikana kwa Taifa letu chini ya serikali ya awamu ya Tano ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli, yenye dhamira ya dhati katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Katika hatua nyingine, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh Benjamini sitta, ameainisha miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Manispaa yake kuwa ni mradi wa soko la magomeni, tandale na ufukwe wa Coco beach, na kuwataka watendaji kuwa mstari wa mbele kuainisha changamoto zinazosababisha kutofikiwa kwa malengo ya miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa kituo cha Afya kigogo, ujenzi wa jengo la madarasa ghorofa mbili sekondari ya mzimuni, ujenzi wa soko la kisasa Magomeni na Zahanati ya Mikoroshini.
Miradi mingine ni Ujenzi wa barabara ya Argentina, mabatini, Mwananyamala, Maboresho ya ufukwe wa coco beach pamoja na daraja la Mkwajuni.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.