Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala alipozuru katika eneo la ujenzi wa kiwanja hicho kinachojengwa kwa kutumia fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri kilichopo eneo la Mwenge katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo pamoja na utatuzi wa migogoro ya Ardhi iliyofanyika leo.
Amesema Kinondoni wamefanya jambo lenye tija kwao na Taifa kwa ujumla kwani kiwanja hiki ni sehemu ya chanzo cha Mapato pindi kitakapokamilika na kuanza kutumika kwa michezo yakiwemo mazoezi ya mpira wa miguu kwa kukodi.
Amesema" Tukubaliane ligi kuu itakayoanza uwanja wetu wa mpira uwepo, ili waweze kufanya mazoezi, kwanza mmeweka vizuri ramani ya ujenzi wa maduka, hii maana yake Mapato." RC Makala.
Ameongeza kuwa Dar es Salaam inayo uhaba wa viwanja vya mazoezi, kwa maana hiyo ni fursa pekee kwani sio lazima kucheza mechi bali hata mazoezi kwa kukodi ikaingiza Mapato.
Pia Mhe. Makala amefurahishwa na hekima za Manispaa ya Kinondoni kuamua kujenga msikiti wa kuabudia kwa waumini wa dini ya Kiislam kwenye eneo la mita za mraba 1000, baada ya msikiti wa sasa kuwa ndani ya eneo la stendi.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Songoro Mnyonge alipofafanua amesema Kinondoni inakwenda kwa kasi na kumhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba kufika ligi kuu kuanza, uwanja huo utakuwa umekamilika katika vigezo vyote.
Katika hatua nyingine Mhe. Makala katika ziara yake amesitisha zoezi la uchimbaji wa kokoto eneo la Boko na kutoa wiki moja kwa wavamizi hao kuondoka eneo hilo, kupisha ujenzi wa kiwanda cha saruji.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.