NI ULE WA UJENZI WA HOSPITALI YA MABWEPANDE KWA GHARAMA YA TSH BILIONI 2.5, MAPATO YAKE YA NDANI HADI KUKAMILIKA KWAKE.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Abubakar Kunenge alipofanya ziara katika Manispaa hiyo ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa Hospitali ya Mabwepande iliyopo katika eneo la Mabwepande Manispaa ya Kinondoni.
Amesema Manispaa hiyo ndiyo pekee kwa Mkoa wa Dar es Salaam iliyoweza kujenga Hospitali kubwa yenye kiwango kinachoridhisha itakayokuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kutumia mapato yake ya ndani.
Amesema "Kinondoni mnafanya vizuri kwa habari ya miradi, mnatafsiri vizuri maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kusogeza huduma karibu na wananchi kwa ujenzi wa hospitali hii na inabidi Halmashauri nyingine zije kujifunza hapa kwenu kwani ndio Halmashauri ya mfano ninayotamani Halmashauri nyingine ziwe" Amesema Kunenge.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mheshimiwa Songoro Mnyonge alipotakiwa kufafanua jambo amesema kuwa Hospitali hiyo ya Mabwepande inayo uwezo wa kuhudumia wagonjwa wa nje 400 hadi 700 kwa siku na wagonjwa wa kulazwa 187 hadi 224 kwa siku.
Aidha Mstahiki Meya pia ameahidi kuyatekeleza maagizo yote aliyopewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Kunenge kwa kushirikiana na watendaji pamoja na kutekeleza mikakati kwa kutenga fedha katika bajeti ya 2021/2122.
Alipotakiwa kuzitaja changamoto zinazoikabili Hospitali ya Mabwepande, Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo Dkt. Christowelu Mande amesema ni ukosefu wa gari ya kubebea wagonjwa hali inayopelekea mazingira magumu wakati wa uhitaji wake.
Katika hatua nyingine Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dkt. Samweli Laiser amesema Hospitali ya Mabwepande inatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi za Kitanzania takribani Bilioni 2.5 hadi kukamilika kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametembelea mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Mabwepande na kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Mabwepande pamoja na Zahanati ya Bunju.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.