Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa kuwa na kusudio la kujenga kiwanda cha kuchakata taka cha mbolea kitakachogharimu takribani shilingi bilioni 4.1 katika eneo la Mabwepande.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda leo alipokuwa akiongea kwenye mkutano na wananchi wa Tandale wanaotakiwa kulipwa fidia kupisha mradi wa DMDP
Amesema mradi huu utakapokamilika utakuwa na faida kubwa Sana kwa nchi yetu. Utaipeleka Dar Es Salaam pale inapotakiwa kuwa kwa swala la usafi wa Mazingira.
Pili utapunguza taka za kwenye masoko, utaongeza mapato kwa Halmashauri ya Kinondoni yatakayotokana na mauzo ya mbolea na utapunguza matumizi ya mbolea zenye kuleta athari ardhi na afya ya binadamu na pia huongeza fursa za ajira kwa vijana wa Kitanzania.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.