Pongezi hizo zimetolewa leo na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe. Stella Ikupa alipotembelea Manispaa ya Kinondoni ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mikoa mbalimbali nchini.
Mhe. Ikupa katika ziara yake hiyo alipata fursa ya kuongea na watu wenye ulemavu waishio Kinondoni ambapo pamoja na mambo mengine ameoneshwa kuridhishwa na utekelezaji wa sera zinazowahusu watu wenye ulemavu waishio katika eneo hilo na kuwahakikishia kuwa yuko bega kwa bega kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji.
"Nitumie nafasi hii kuupongeza sana uongozi wa Manispaa hii ya Kinondoni kwa jinsi ambavyo mnashughulikia masuala ya watu wenye ulemavu na kwa Jinsi ambavyo mmejipanga kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowahusu watu wenye ulemavu" Amesema Naibu waziri Ikupa.
Awali akitoa taarifa ya Manispaa ya Kinondoni, Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dkt Ezra Ngereza amesema katika bajeti Ijayo ya mwaka 2019-2020 , Manispaa imetenga kiasi Cha shilingi Mil 9 kwa ajili ya kuwatambua na kuwapa kadi za msamaha wa matibabu watu wenye ulemavu.
Aidha kiasi cha shilingi Mil 50 kimetengwa kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya kununulia vifaa visaidizi vya watu wenye ulemavu huku vikundi mbalimbali vya ujasiriamali vya watu wenye ulemavu vikiwezeshwa kupatiwa mkopo.
Katika hatua nyingine Naibu waziri ameshauri zoezi la uundwaji wa Kamati za watu wenye ulemavu kwa ngazi ya Kata na Mitaa likamilike kwa uharaka zaidi ili waweze kupata wasaha wa kujadili mambo yanayowahusu na kutatua changamoto zao zinazowakabili.
Kwa upande wao watu wenye ulemavu wameainisha changamoto kubwa wanazokutana nazo kuwa ni pamoja na ufinyu wa maeneo ya kufanyia biashara, uhaba wa maeneo ya mazoezi, usumbufu kwenye vyombo vya usafiri, changamoto ya bima ya afya, na baadhi ya walemavu kuficha watoto wenye ulemavu.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.