Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa juhudi walizozifanya usiku na mchana kuhakikisha miundombinu ya soko la Bunju B lililopo Bunju Kata Ya Mabwepande inakamilika kwa wakati.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ali Hapi alipokuwa akizindua choo chenye matundu kumi na mbili sokoni hapo.
Amesema Mkurugenzi pamoja na watendaji wake wamefanya kazi usiku na mchana kuhakikisha miundombinu hiyo inakamilika kwa ubora uliokubalika.
"Nampongeza Mkurugenzi, pamoja na watendaji wake, wamefanyakazi kwa muda mfupi, usiku na mchana kuhakikisha miundo mbinu hii inakamilika kwa ubora uliokusudiwa" Amesema Hapi.
Akiitaja miundombinu hiyo kuwa ni choo, maji, umeme pamoja na eneo la machinjio yenye uwezo wa kuandaa kuku zaidi ya elfu moja kwa mara moja, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kukamilika kwake kutasaidia wafanyabiashara kufanya kazi zao kwenye Mazingira bora na salama.
Ameongeza kuwa wakati umefika sasa kwa wafanyabiashara Wale waliokuwa barabarani kurudi sokoni kwani kwa kufanyabiashara maeneo ya barabarani ni kuhatarisha maisha na pia ni kinyume cha sheria.
Ametoa rai kwa wafanyabiashara kuwa wazalendo, kuilinda, kuipenda, kuithamini miundombinu yote hiyo ili iweze kutumika na kuleta faida si tu kwa wao bali na kwa vizazi vijavyo.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.