NI KATIKA KUIENZI SIKU YA MASHUJAA INAYOADHIMISHWA TAREHE 25/07, KILA MWAKA.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa usafi eneo la fukwe za coco beach kama ishara ya kuwaenzi mashujaa wetu siku inayoadhimishwa tarehe 25/07, kila mwaka.
Amesema kufanya usafi eneo la fukwe ni maamuzi ya busara yenye kutambua umuhimu na kuyaenzi maeneo ambayo ni maalumu na ya kimkakati si tu kwa Taifa la Tanzania, bali kwa wananchi watumiaji wa maeneo hayo.
"Maamuzi yenu Mkoa wa Dar es Salaam, maamuzi yenu Wilaya ya Kinondoni ya kuja kuuweka vizuri ufukwe wetu wa koko, ambao kwa sasa ni ufukwe maarufu nchini, unaokusanya watanzania wengi kuja kupumnzika hasa nyakati za jioni, Jambo hili ni jambo la busara Sana "Amebainisha Majaliwa .
Aidha ameongeza kuwa eneo hili kwa sasa ni eneo la kimkakati, ambalo ni kivutio kikubwa kwa wageni wa ndani na nje ya Nchi, hivyo hakuna budi kuhakikisha linaboreshwa, ulinzi unaimarishwa, na usafi unafanyika ili liweze kuleta tija kwa watumiaji.
Awali akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ali Hapi amesema kupitia miradi ya kimkakati Halmashauri iliona fursa katika eneo la fukwe hii na kuomba kiasi cha fedha za kitanzania tsh bilioni 11, kwa ajili ya kulitengeneza na kuliboresha eneo hilo ambalo limekuwa kivutio kwa watanzania.
Zoezi hili la usafi lililoenda sambamba na uboreshaji wa Mazingira kwa kupanda miti, pia limehudhuriwa na viongozi wa vyama na Serikali, vikundi vya jogging, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na Wilaya, pamoja na wakuu wa idara na vitengo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.