NI KATIKA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM KATIKA KUIMARISHA MIUNDOMBINU SEKTA
Manispaa ya Kinondoni imepokea vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni saba kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa Masokoni.
Vifaa hivyo vimepokelewa leo katika ukumbi mdogo wa Elimu wa Manispaa ambapo wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyabiashara wa masokoni walikuwepo.
Akikabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa MUMADA ndugu Mohamed Mwekya amesema hatua hii ni katika kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh Paul Makonda za kuimarisha miundombinu ya sekta ya elimu kwa kujenga majengo ya utawala na vyoo katika shule za Msingi na Sekondari ili kuandaa Mazingira mazuri ya walimu katika shule hizo.
Amevitaja vifaa walivyovikabidhi kwa Manispaa hiyo kuwa ni Mchele kilo 2835, Maharage kilo 630, pakiti za chumvi pamoja na vifaa vya usafi.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Mwajuma Magwiza ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya jamii amewapongeza na kuwashukuru wadau wote walioguswa na kuunga mkono jitihada hizi za Mkuu wa Mkoa za kuondoa changamoto katika sekta ya Elimu.
Amesema "kama Manispaa ya Kinondoni tunawashukuru sana wafanyabiashara wetu, na tunafurahi kuona kwamba wapo mstari wa mbele kushirikiana nasi kwa kila jambo na pia ni wadau wenye nia njema kabisa ya kuona miundombinu ya sekta ya elimu inaimarika"
Ametoa wito kwa wadau wengine walioguswa kuendelea kushirikiana nasi katika kufanikisha Jambo hili kwa kujitokeza na kutoa michango yao ya hali na mali.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.