Vifaa hivyo vimepokelewa toka shirika la kulinda watoto la save the children kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wanakuwa salama kwa wakati huu ambao wamerudi shuleni kuendelea na masomo yao.
Akiongea wakati wa kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispa, Mganga Mkuu wa manispa Dkt Samwel Laiza amelishukuru shirika la save the children kwa kuwezesha kupatikana kwa vifaa hivyo kwani vifaa vilivyopo sasa havitoshelezi mahitaji halisi ya wanafunzi.
"Tunawashukuru Ndugu zetu hawa sababu wameona Kuna umuhimu wa kuwakinga watoto wetu kwani corona Bado ipo japo imepungua Sana, lakini Kama jamii Bado inatakiwa kuchukua tahadhari zinazoshauriwa na wataalamu wetu"
Amesema Dkt Laiza
Ameongeza pia kinondoni Ina mkakati wa kufanya zoezi la unawaji mikono kuwa endelevu hata baada ya kuisha kwa mlipuko wa ugonjwa wa corona kwani tafiti zinaonesha kwa kunawa mikono kunapunguza asilimia 60 ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya mfumo wa chakula.
Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa uchechemuzi na kampeni wa shirika la save the children Bi Nuria Mshare amesema kuwa wao kama shirika Wana wajibu wa kuhakikisha watoto wanakuwa salama , hivyo wameguswa kuhakikisha watoto wa Shule wanakuwa salama wakiwa shuleni kwa kuwapatia vifaa vitakavyowawezesha kutakasa mikono Yao wakati wote watakaokuwa wanaendelea na masomo.
Amesema shirika liko begakwabega na serikali kuhakikisha mapambano dhidi ya virusi vya corona kwa wanafunzi yanafanikwa na wanafunzi wanaendelea na masomo Yao bila ya kuwa na usumbufu wowote.
Naye mwalimu mkuu wa Shule ya secondari ya Kigogo Mwl Ester Idabu amesema awali walikuwa na changamoto ya vifaa vya kunawia ambapo walikua wanatumia ndoo za kawaida hali iliyowalazimu kujaza maji kila baada ya muda fulani lakini kwasasa baada ya kupata matanki hayo makubwa yatapunguza isumbufu huo.
Afisa elimu Msingi anaeshughulika na masuala ya afyaeza wanafunzi Bi Martha Kusaga amesema vifaa hivyo vitagawiwa kwa shule kumi ambazo ni kisauke ( Msingi na sekondari), Sekondari za Kigogo, mikocheni, Kawe na Bunju pamoja na shule za Msingi za Changanyikeni, Salasala, Mbezi Ndumbwi pamoja na makongo juu.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Matanki ya maji 20, Sabuni za kunawia mikono 500, Taulo za kike 1000 na Nguo za ndani 500.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.